MAKUBWAA..!! TAZAMA JINSI MSANII "RECHO" ALIVYOVAA STEJINI, NI VAZI GANI HILI..??

 Ni tatizo! Sexy lady wa Bongo Fleva, Winfrida Josephat ‘Recho’ ametia fora baada ya kutinga kipensi kilichoonesha sawia maungo yake nyeti.
...Akizidi kufanya yake.
Ishu hiyo ya aibu ilijiri kwenye Ukumbi wa Sun Ciro uliopo Ubungo, Dar ambapo kulikuwa na kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kilichopo Dar huku Recho akiwa mtumbuizaji.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, Recho alipanda kwa steji kupiga shoo akiwa ametinga kivazi hicho ambacho kilikuwa ni sawa na ‘kufuli’ hivyo kuibua gumzo kwenye shindano hilo ambalo aliyeibuka kidedea ni Junis Ndalima.
Baadhi ya wanachuo wa Ustawi walionesha kushangazwa na tukio huku wakiweka wazi kuwa msanii huyo ni tatizo.
Ijumaa Wikienda lilipomfuata kutaka kujua kulikoni ‘kutokelezea’ mbele za watu na kipisi hicho cha kipensi hakuwa na jibu.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI
BOFYA “LIKE” HAPO CHINI KUPATA HABARI ZETU..!!

0 comments: