BONGO MOVIE HAPAKALIKI , KILA KUKICHA UGOMVI ,BIFU LA RAY NA JOHARI HADI MSIBANI CHEKI HAPA
Ishu! Wakurugenzi wa Kampuni ya RJ Productions, waliowahi kudaiwa
kutoka kimalovee, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’
wametoa kali ya katika Makaburi ya Kinondoni, Dar, wakati wa mazishi ya
mwigizaji mwenzao, Sheila Haule ‘Recho’ baada ya kuombwa kwa pamoja
wainuke kuweka shada kaburini lakini wao wakachengana.
Wakurugenzi
wa Kampuni ya RJ Productions, waliowahi kudaiwa kutoka kimalovee,
Vincent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’ wakiweka shada za maua
kaburini,kila mmoja kivyake bila ya umoja wowowte.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, MC Salum Mchoma ‘Chiki’ alisikika akisema kuwa sasa ni zamu ya watu kuweka mashada spesho ndipo akawainua mastaa hao ambapo Ray baada ya kusikia jina lake alionekana kushtuka kidogo kabla hajachukua uamuzi wa kwenda kuweka shada hilo.
Badala ya kuchukua shada moja kila mmoja alichukua lake huku kila mmoja akimchenga mwezake.
0 comments: