BIFU ZITO LA DIAMOND PLATNUM NA ALI KIBA LAJA KWA STAILI MPYAA..Hii ndiyo Kauli Ya Kusaga Wa Clouds Media Group Juu Ya Bifu Hilo.

ALIKIBA
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema atajaribu kukaa na wasanii wa muziki Diamond na Ali Kiba na kuangalia tofauti zao ili kuwapatanisha.
Akizungumza na The Sporah Show hivi karibuni, Kusaga amedai kuwa alikuwa hatambui kama wasanii hao wana matatizo kwenye kazi zao na kuahidi kuwa ataliangalia tatizo lao.
“Kiukweli wote ni watoto wangu, Diamond ananipa heshima sana mimi ,namshukuru, Ali Kiba is the same, nafanya nao kazi na sijawahi kugombana nao. Lakini sijui kama walikuwa wana tatizo ndo nasikia sasa, lakini ngoja nijaribu kuwapigia ni find out kwanini? na kuna tatizo gani between wao, lakini sijawahi kujua wana matatizo hayo.”
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI
BOFYA “LIKE” HAPO CHINI KUPATA HABARI ZETU..!!

0 comments: