BAADA YA KUTESWA SANA NA MAPENZI, MSANII RAY C AFUNGUKA NA KUFANYA MAAMUZI MAZITO...!! SOMA HAPA KUYAJUA
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu, na kama ikitokea basi atamtaka kuwa na miaka kuanzia 60.
Akizungumza katika kipindi cha ‘The Sporah Show’, Ray C alisema
anahitaji wanaume wa umri mkubwa, kwa kuwa wanajua wanachokifanya, na
kukiri kwamba vijana walichangia katika kurudisha nyuma maisha yake.
Msanii huyo ambaye kwa sasa ameanzisha asasi yake ya kupambana na
dawa za kulevya, kutokana na yeye kuwa mmoja wa waathirika wa dawa hizo,
alisema katika moja ya mambo anayoyajutia ni kuwa na mahusiano na
vijana, jambo ambalo hataki kukumbuka walichomfanyia hadi kudhalilika
mbele ya jamii.
Hata hivyo, alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi kutowatenga watoto wao
ambao wamejidumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya na badala
yake, wawakumbatie na kuwaonyesha njia kama mama yake alivyofanya na
kurudia hali yake ya kawaida.
Kuhusu kurudi kwenye muziki, Ray C alisema yupo mbioni na tayari
ameshatengeneza nyimbo kadhaa, ambapo hivi sasa atakuwa akiimba miondoko
tofauti tofauti, ikiwemo taarabu.
Katika kurudi kwenye muziki, jambo la kwanza alisema anatarajia
kupunguza mwili wake kwa kufanya mazoezi, kwani hata daktari wake
alishamwambia anatakiwa kupungua kutokana na umri wake kutoendana na
kilo alizonazo.
Alipoulizwa mwanamuziki ambaye kwa sasa anamkubali Bongo, Ray C
alisema wa kwanza ni AT akifuatiwa na Recho kutoka Jumba la Kukuza
Vipaji (THT).
0 comments: