NECTA YABADILI VIWANGO VYA UFAULU FORM 6, DIV 1 MWISHO POINT 7..SOMA ZAIDI HAPA
NECTA imetoa mwongozo wa matumizi ya viwango vya Ufaulu (Aprili 2014)
ambao umesambwazwa katika shule zote ze sekondari kupitia kwa Maafisa
Elimu wa Mikoa. Kwa mujibu wa mwongozo huo Madaraja ya ufaulu kwa Kidato
cha Sita 2014 yatapangwa kwa kutumia mfumo uliooneshwa kwenye ukurasa
wa 8 wa mwongozo huo ambao ni:
Div I pointi 3-7
Div II pointi 8-9
Div III Pointi 10-13
Div IV awe na D mbili au C moja
Div 0 aliyepata chini ya D mbili.
Kwa mujibu wa mwongozo huo masomo yatakayohesabika kwenye kupanga pointi
ni yale tu yaliyoko kwenye tahasusi yaani combination. Kwa maneno
mengine suala la kupata cheti kwa mgongo wa Bible Knowledge au Islamic
Knowledge litakuwa halipo tena.
Kuanzia Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Tano Sita 2015 mfumo wa GPA
utatumia. Kwa maelezo Zaidi soma kurasa wa 8 na 9 na pia unaweza
kukipata kijitabu hicho toka shule yoyote ya sekondari au kwenye ofisi
za elimu za mkoa na wilaya.
0 comments: