MATUKIO KATIKA PICHA..!!TAZAMA AJALI ALIYOPATA WALTER CHILAMBO WA BSS JANA SAA TANO USIKU
Ajali
imetokea saa sita kasoro usiku May 15 2014 Kimara Dar es salaam ambapo
mwimbaji Walter ambae ni mshindi wa BSS 2013 akiwa barabarani
anaendesha alipata mshtuko mkubwa baada ya gari iliyokua nyuma yake
kuja kwa kasi na kumchomekea kwa mbele na kumsukuma.
Kwa
mlio uliotokea na jinsi tukio lenyewe lilivyokuwa Walter alipata
mshtuko na kupanic kwa muda kabla ya kuanza kurejea kwenye hali yake
kutokana na ajali hii ambayo haikumpa jeraha lolote.
Kwa jinsi jamaa wa gari jingine alivyomvamia unaweza kuhisi labda alikua anayo nia ya kumuumiza Walter au alipania kumgonga isivyo kawaida manake toka alipokuwa nyuma ya Walter alikua akimuwashia taa kwa mwanga mkubwa kuashiria anataka kupita.
Baada
ya kumwashia Walter taa kwa muda mrefu ilipopatikana nafasi ya
kumpisha alimwachia ila kabla hajapita huyu jamaa aliekua na wenzake
wanne walifungua vioo na kuanza kumtukana Walter kisha akamchomekea
mbele kwa makusudi ndio Walter akagonga mbele kisha ukuta wa barabara
na bampa likaingia chini ya matairi na jamaa wale wakakimbia bila
Walter kuweza kushika hata namba za gari.
Walter anasema ‘wale jamaa ilikua kama wanakimbizwa huko walikotoka’
Uwapo
barabarani Dar es salaam unashauriwa kumpisha yeyote anaetaka kupita
kama kuna nafasi, Mwaka jana kuna dereva wa daladala aliuwawa kwa risasi
na watu waliokua kwenye pikipiki waliotaka awapishe lakini akawa
anawanyima nafasi ambapo walipopata upenyo wa kumpita eneo la Sinza
Kumekucha jamaa aliekua kapakiswa kwenye pikipiki alifyatua risasi
iliyomuua palepale dereva wa daladala.
Kabla ya kumuua yalitokea majibizano kidogo ambapo iliripotiwa Dereva wa daladala kama kawaida yao akajibizana nao na kuwauliza watamfanya nini, wasepe zao waache kumbabaisha.
Kwa jinsi jamaa wa gari jingine alivyomvamia unaweza kuhisi labda alikua anayo nia ya kumuumiza Walter au alipania kumgonga isivyo kawaida manake toka alipokuwa nyuma ya Walter alikua akimuwashia taa kwa mwanga mkubwa kuashiria anataka kupita.
Baada
ya kumwashia Walter taa kwa muda mrefu ilipopatikana nafasi ya
kumpisha alimwachia ila kabla hajapita huyu jamaa aliekua na wenzake
wanne walifungua vioo na kuanza kumtukana Walter kisha akamchomekea
mbele kwa makusudi ndio Walter akagonga mbele kisha ukuta wa barabara
na bampa likaingia chini ya matairi na jamaa wale wakakimbia bila
Walter kuweza kushika hata namba za gari.Walter anasema ‘wale jamaa ilikua kama wanakimbizwa huko walikotoka’
Uwapo
barabarani Dar es salaam unashauriwa kumpisha yeyote anaetaka kupita
kama kuna nafasi, Mwaka jana kuna dereva wa daladala aliuwawa kwa risasi
na watu waliokua kwenye pikipiki waliotaka awapishe lakini akawa
anawanyima nafasi ambapo walipopata upenyo wa kumpita eneo la Sinza
Kumekucha jamaa aliekua kapakiswa kwenye pikipiki alifyatua risasi
iliyomuua palepale dereva wa daladala.Kabla ya kumuua yalitokea majibizano kidogo ambapo iliripotiwa Dereva wa daladala kama kawaida yao akajibizana nao na kuwauliza watamfanya nini, wasepe zao waache kumbabaisha.

0 comments: