JAHARI AWEKA MAMBO WAZII..! AAMUA KUFUNGUKA JUU YA SKENDO ZAKE ZOTE KUHUSU RAY NA KUPORA MUME WA MTU..


WIKI iliyopita mwandishi wetu Sifael Paul alianza kuweka wazi kile alichozungumza na msanii maarufu wa filamu Bongo, Johari. Mahojiano hayo yanaendelea tena leo, ungana naye:
Sifael: RJ inamilikiwa na Johari na Ray, je, mgawanyo wa mapato ukoje?
Johari: Tunagawana kwa usawa.
Sifael: Kuna taarifa kuwa Ray anachukua kipato kikubwa kuliko wewe, je, ni kweli?
Johari: Si kweli. Kila mtu anapata sawa.
Sifael: Kuna stori mtaani kuwa mnataka kugawana kampuni kila mtu achukue hamsini zake. Je, ni kweli?
Ray: Hakuna jambo kama hilo.
Unajua misingi ya RJ ni imara sana. Siyo ya kusambaratika kirahisi hivyo.
Sifael: Uhusiano wako na Ray upoje?
Johari: Ni mkurugenzi mwenzangu au vipi?
Sifael: Uhusiano wenu wa kimapenzi upoje?
Johari: Nimekwambia ni mkurugenzi mwenzangu, unataka nini tena?
Sifael: Hana mpango wa kukuoa?
Johari: (kicheko cha kufa mtu) hatuna mipango kama hiyo, hapa kazi tu.
Sifael: Upo tayari kumuona Ray anamuoa mwanamke mwingine wakati mmekuwa pamoja kwa muda mrefu?
Johari: Tena nikwambie siri, mimi ndiye nitakuwa mwenyekiti wa kamati ya harusi ya Ray. Yaani nitasimamia vikao vyote vya harusi ya Ray. Nakwambia nitakuwa mstari wa mbele hadi nionekane kiherehere kabisa.
Sifael: Kama siyo Ray, mchumba wako ni nani?
Johari: Yupo, ni mtu ambaye nikikutajia utashangaa lakini siwezi kumtaja kwa sasa.
Sifael: Au ni Ostaz Juma ambaye anatangaza anataka kukuoa?
Johari: Siyo na sitaki kumzungumzia huyo mtu.
Sifael: Unataka mchumba’ko awe na sifa gani?
Johari: Kijana mchapakazi, mpole, anayejituma katika maisha.
Sifael: Tangu umevunja ungo umewahi kutoka kimapenzi na wanaume wangapi?
Johari: Siwezi kujibu hilo.
Wewe niulize filamu mpya inayotoka au wasanii wangapi nimewatengeneza.
Sifael: Bongo Movies mnasifika kwa tabia ya kuchukuliana wanaume. Je, hilo unalizungumziaje?
Johari: Si wote.
Ni baadhi ya watoto wa kike wenye tamaa ya kutaka vya bure jambo ambalo ni baya sana. Ni akili ya mtu tu. Katika maisha kila mtu ana hulka na tabia yake.
Sifael: Je, wewe hujawahi kukumbwa na skendo ya kupora mume wa mtu?
Johari: Mimi? Haijawahi kutokea.
Sifael: Wewe ni Mkristo, wasanii wengi hawaendi kanisani, mara ya mwisho wewe kwenda kanisani ni lini?
Johari: Jumapili iliyopita.
Sifael: Ni filamu gani ya kwako unaipenda?
Johari: Ni Bad Lucky.
Sifael: Kwa nini?
Johari: Naipenda kwa sababu nimeigiza na Baba Haji, Batuli, Salha Israel na Dullah wa Planet Bongo.
Sifael: Mara kwa mara umekuwa ukiripotiwa kuwa mgonjwa. Unaizungumziaje afya yako?
Johari: Afya yangu ipo poa kabisa (akinyanyuka na kuongeza kiyoyozi).
Sifael: Una mtoto?
Johari: Sina.
Sifael: Ulishatoa mimba?
Johari: Hapana, najua ni dhambi na ni kosa kubwa kuua kiumbe asiyekuwa na hatia.
Sifael: Julai 28 (nyota ya simba), mwaka huu unatimiza umri wa miaka 31. Umri umekwenda. Je, hutamani kuwa na mtoto?
Johari: Kwanza mimi napenda sana watoto. Muda ukifika nami nitakuwa na wa kwangu. Ishu hapa ni muda tu, ukifika freshi.
Sifael: Katika kipindi chote ulichofanya sanaa umepata mafanikio gani?
Johari: Unamaanisha utajiri au fursa?
Sifael: Vyote.
Johari: Kama hivi tuna kampuni na ofisi nzuri tofauti na wasanii wengine ambao wana kampuni lakini hawana ofisi. Nina usafiri mzuri, nina mahali pazuri pa kulaza mbavu. Naendesha maisha yangu vizuri. Ukweli sina fedha lakini nina makaratasi kidogo. Lakini hiyo yote haitokani na filamu tu. Nina biashara nyingine ndogondogo.
Sifael: Nini malengo yako? Miaka mitano ijayo?
Johari: Ni kuongeza bidii na kuipeleka tasnia yetu kimataifa pamoja na kuwa na familia bora. Ifahamike pia mimi ni super woman mtafutaji ile mbaya.
Sifael: Neno la mwisho kwa mashabiki wako na Watanzania kwa ujumla ni lipi?
Johari: Tuongeze bidii katika kutafuta fedha kwa njia halali. Nawapenda wote.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI
BOFYA “LIKE” HAPO CHINI KUPATA HABARI ZETU..!!

0 comments: