HATIMAYE VIGODORO KUPIGWA MARUFUKU JIJINI DAR ES SALAAM..
Jeshi
la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku ngoma za
kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika nyakati za usiku kwenye maeneo
mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana makundi ya
kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia.
Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa watu, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema ‘ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za usiku’

Kamanda
Kova anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo
vya kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya mia moja
ambapo pia watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu
vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama
‘vigodoro’ pamoja ‘baikoko’ na sasa jeshi la polisi limetoa onyo kali
kwa watakaoendeleza hizi ngoma kuanzia sasa.
0 comments: