DUU USWAHILINI KUNA VITUKO..!! AKODI NGOMA KUMFUMANIA MKE! MTAA WAFUNGWA KWA CHEREKO CHEREKO,POLISI WAINGILIA KATI, BAKI NJIA KUU MICHEPUKO SIO DILI
AMA kweli dunia ina mambo na mambo yenyewe ndiyo haya! Katika hali ya kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ramadhan
Ally, mkazi wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amewashangaza wengi
kufuatia uamuzi wake wa kukodi ngoma ya asili kwa lengo la kwenda
kumfumania mkewe aliyejulikana kwa jina moja la Asha.
Tukio
hilo lililofunga mtaa lilijiri asubuhi ya saa 3:14 Jumatatu iliyopita
eneo maarufu kwa jina la Sultani baada ya mwanaume huyo kutonywa kuwa,
mke wake alikuwa amelala kwa rafiki yake kipenzi, Abdallah Elias.
Baadhi
ya wananchi waliobahatika kuwasili katika eneo la tukio walishuhudia
mwenye mali akiwashushia kichapo kikali ‘wasaliti’ hao ambapo vurugu
zikapamba moto.
Kufuatia
hali hiyo, viongozi wa serikali ya mtaa huo waliamua kutoa taarifa kwa
Kamanda Mkuu wa Ulinzi wa Jadi Kata ya Mbuyuni, Aidan Mtimbo ambaye
alifika eneo la tukio na vijana wake na kuwasomba watuhumiwa hao
msobemsobe huku wakisindikizwa na ngoma hiyo hadi Kituo cha Polisi Kata
ya Mbuyuni.
Katika
hali ya kushangza, nje ya kituo hicho cha polisi baadhi ya wananchi
waliokuwa na hasira walishinikiza watuhumiwa watolewe nje wawafanyie
kitumbaya huku baadhi yao wakikipopoa mawe kituo hicho kilichokuwa na
askari mmoja aliyevaa nguo za kiraia.
Baada
ya vurugu hizo, afande huyo alipiga simu kituo kikuu cha polisi kuomba
msaada ambapo askari wa pikipiki walifika na kuwakodia teksi watuhumiwa
hadi kituoni.
Mwandishi
wetu alifanikiwa kuwahoji wahusika wote watatu ambapo mume wa mwanamke
huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza kama ifuatavyo:
“Huyu mwanamke ni malaya sana, kwanza nimemtoa kwao Matombo (Morogoro) akiwa na watoto wawili na kila mmoja na baba yake.
“Mimi sikujali hilo, ukipenda bonga penda na ua lake.
Miezi mitatu iliyopita aliniambia ana ujauzito wangu, taarifa hizo
zilinifurahisha sana. Cha ajabu juzi akaniambia ametoa mimba yangu,
nilipomuuliza kwa nini, akasema kwa ujeuri eti hayupo tayari kuzaa na
mimi kwa sasa.
“Nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao, jana usiku napokea taarifa kuwa yuko nyumbani kwa rafiki yangu kipenzi, Abdallah Elias.
Polisi baada ya kutinga eneo la tukio kuwanusuru watuhumiwa.
“Ndiyo asubuhi nikakodi ngoma na kwenda, niliwakuta wamelala kitandani.”
Kwa upande wake Elias alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema:
“Huyu mwanamke ni mbaya sana, ametuchanganya mimi na rafiki yangu Dullah, yeye kaja kwangu jana Jumapili akaniambia amefukuzwa na mumewe hivyo anaomba alale kwangu kesho yaani leo aende kwao Matombo kumbe alisharudishwa kwao toka juzi.”
Kwa upande wake Elias alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema:
“Huyu mwanamke ni mbaya sana, ametuchanganya mimi na rafiki yangu Dullah, yeye kaja kwangu jana Jumapili akaniambia amefukuzwa na mumewe hivyo anaomba alale kwangu kesho yaani leo aende kwao Matombo kumbe alisharudishwa kwao toka juzi.”
Naye mwanamke huyo alipohojiwa na paparazi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Huyu mwanaume (Ramadhan) hajanioa, kila siku nikimwambia twende kwa wazazi wangu ananipiga danadana. Ni kweli nimetoa mimba yake, siko tayari kuzaa naye mtoto nje ya ndoa. Huyu Elias, yeye alionesha nia ya kunioa.”
“Huyu mwanaume (Ramadhan) hajanioa, kila siku nikimwambia twende kwa wazazi wangu ananipiga danadana. Ni kweli nimetoa mimba yake, siko tayari kuzaa naye mtoto nje ya ndoa. Huyu Elias, yeye alionesha nia ya kunioa.”
Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel
Msuya amethibitisha kutokea kwa fumanizi hilo kwenye mtaa wake lakini
aliwatupia lawama polisi wa pikipiki kwa kupuuza uongozi wa juu wa kata
hiyo ambao kwa kushirikiana na walinzi wa jadi walifanikiwa kuwalinda
watuhumiwa wao na kufika salama kwenye kituo cha polisi.
0 comments: