STORI YA KUHUZUNISHA..!! KUTANA NA MREMBO ALIYEAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI NA MWANAMKE MSAGAJI..SOMA STORI YOTE HAPA
Zuwena ( sio jina lake halisi ), ni mwanamke wa kitanzania mwenye umri wa miaka 43. Kwa sasa mwanadada huyu anaishi na virusi vya ukimwi.
Mwanadada huyu anabainisha namna alivyo pata maambukizi
ya VVU kwa kujamiiana na mwanamke mwenzake, ama kwa lugha
nyingine, Zuwena anaeleza namna ambavyo mwanamke msagaji
alimuambukiza v.v.u wakati wakiwa na uhusiano wa jinsi
moja...
Fuatilia kisa hiki cha kufundisha na kusikitisha.
"Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2007,
nilipata tenda ya u MC katika sherehe ya kumuaga binti wa jirani yangu kule Buza
Cape Town. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mihogoni Pub kulekule
Buza.
"Saa moja usiku nilikuwa nimeshafika ukumbini na kutoa
maelekezo kwa wageni waalikwa, watu walikuwa wengi kiasi ambacho hata mama
mwenye sherehe alifurahi kwa jinsi watu walivyo muitikia. Kama kawaida
niliendelea na matangazo ya hapa na pale, watu walicheza na
kufurahi.
"Muda wa chakula ulipowadia nilikaa pembeni nikiwa
naangalia watu wanavyo kwenda kuchukua chakula. Ghafla alitokea mama mmoja mtu
mzima kwa kumkadiria alikuwa na miaka kama 48 – 50 hivi.
"Alinifata pale nilipokuwa nimesimama na kuanza kutoa
sifa za hapa na pale mara umependeza , mara unaongea vizuri, mara vazi ulilovaa
limekupendeza, mwisho aliniomba namba ya simu akaniambia kuwa ana sherehe ya
kumuaga binti yake kwa hiyo angependa niwe MC katika shughuli
yake.
"Kwa kweli mimi nilikuwa kazini, sikukataa kumpa namba
yangu. Kesho yake alinipigia simu ya kunisalimia, kwa kuwa kiumri alinizidi
nilimuamkia, ila nilichokisikia masikioni mwangu ni neno ' Ahsante baby
'.
"Nilishituka lakini nikaona ni vitu vya kawaida , kadri
siku zilivyokwenda tulizidi kufahamiana nilimwambia kuwa nina saluni yangu,
alinitumia vocha na mwisho alliniambia anataka kuja kupajua ofisini kwangu,
nilimuelekeza akawa anakuja kutengeneza nywele, akitoa 10,000/= nikimrudishia
chenji ananiambia “ utakunywa soda “ , siku nyingine anafika ofisini kwangu
ananipa hela anaondoka.
"Nikaanza kuwa na mawazo juu ya huyu mama lakini
sikupata jibu. Siku moja akanipigia simu akaniambia anataka kufungua saluni
yake, kwa hiyo angeomba tukutane Cape Town Bar tuongee mimi na yeye. Ilikuwa
siku ya Jumapili, wateja walikuwa wengi alinisubiri kama saa moja
akanipigia
kuniulizia nimekwama wapi? Nikamwambia bado nina wateja
,akaniambia funga saluni njoo nikulipe hela ya siku hiyo
yote.
"Nilifika pale akaniagizia kinywaji na baada ya hapo
akatoa shilinge 50,000/= . Nilishindwa kumuelewa huyu mama akaanza kunihoji
naishi na nani, nikamwambia naishi na watoto wangu watatu, baba yao baba yao
amefariki miaka miwili iliyopita . Nikamuuliza saluni anataka kufungulia
wapi?
"Akanijibu achana kwanza na mambo hayo tutaongea
baadaye . Tuliendelea kunywa hadi saa mbili usiku nikamwambia nawawahi watoto
wangu nyumbani akaniambia nitakupeleka na gari, kusema kweli sikuelewa nia yake
ni nini hivyo hata nyumbani kwangu sikutaka apajue.
"Nilimuaga tena kwa mara ya pili akaniruhusu , kesho
yake aliniletea viroba vya unga na mchele akavishusha saluni kwangu, akaniambia
atanipigia simu kesho yake kuna kitu anataka
kunieleza.
"Nilianza kupata hofu, ilibidi niwaeleze rafiki zangu
wa karibu ,ushauri walionipa waliniambia usikubali kutoka naye kwenda popote
mbali ya pale Buza kwa sababu nia yake hatuielewi.
"Kesho yake akafika pale bar akanipigia simu, nikaenda
ila nikapanga na rafiki yangu mmoja anifuate pale . Alipokuja nilitoa hela ili
nimuagizie kinywaji, Yule mama alinizuia akatoa hela na kumuambia muhudumu alete
kinywaji ila alimuomba yule rafiki yangu akae meza
nyingine.
"Kusema kweli alizidi kunichanganya, sikumuelewa.
Yule
rafiki yangu alikunywa bia ya kwanza na ya pili na
akaja kutuaga akaondoka. Nilimtumia meseji kuwa asicheze
mbali.
"Baada ya kama lisaa limoja hivi alipigiwa simu,
akaniaga akatoa Sh. 10,000/= akanibusu akaondoka. Yaani hapo ndipo alinifanya
niwe na mawazo sana, nikaenda kuwahadithia wenzangu ....wengine wakasema labda
ni msagaji, wengine wakasema ametokea kukupenda tu au anataka kaka yake
akuoe.
"Kesho yake akaja na dereva mwanamke, binti mdogo
mwenye umri kati ya miaka 20 au 25, akaniambia nimsindikize mjini nikamchagulie
nguo za biharusi mtarajiwa.
"Tukaondoka wote hadi Kariakoo, akamwambia Yule dada
apaki gari pembeni ili akajisaidie, Yule binti akajitambulisha kwangu kuwa
anaitwa Angel, akaniuliza huyu mama mmeanza kufahamiana toka lini, nikamwambia
yapata mwezi mmoja sasa.
"Nikamuuliza mbona unaniuliza hivyo akaniambia nilikuwa
nakuuliza tu. Akaniuliza unajishughulisha na nini , nikamwambia nina saluni na
ni MC, akaniomba namba ya simu, Yule mama alipokuja akatuuliza mlikuwa mnaongea
nini? Mimi nikamjibu kuwa dereva wako ananiuliza ile saluni ni yangu au
nimeajiriwa ?
"Tukaja mpaka mtaa wa Tandamti akamwambia apaki gari
atusubiri, tukaanza kuingia madukani, badala ya kutafuta nguo ya bi harusi akawa
ananiambia mimi nichague nguo niliyoipenda nikawa namkatalia , tukaja mpaka mtaa
wa Agrrey kuna duka linauza nguo za kutokea usiku, tukaingia pale kuna nguo
nzuri tuliikuta inauzwa 120,000/= akaniambia niichukue nikakataa, tulipotoka nje
kuna kaka alikuwa anauza viatu simple akaniambia nichague nikaona nisimkatishe
tamaa nikachagua naye akachagua , Mara ikaingia meseji kwenye simu yangu ,
meseji ilikuwa inasema hivi “ Huyo mama unamtambua vizuri au haumtambui, ni
msagaji mzuri pole Aunty nakuhurumia, “ by Angel .
"Kwa kweli nilishtuka nikahisi nazimia , akaniambia
mbona umesoma sms ukaonekana umeshtuka . Nikamwambia kaka yangu amenitumia sms
mtoto wake anaumwa sana.Akaniambia twende nikupeleke , akili yangu ilishahama,
nilimuambia tu hapana acha niende nikapande daladala niwahi
hospitali.
"Alitoa shilingi 10,000/= akanipa kama nauli, nilitoka
speed mithili ya mshale, nilivuka mtaa wa uhuru, nusu nigongwe na gari,
sikuamini macho yangu, nilifungua tena ile sms nikaisoma , ghafla akanitumia
vocha ya sh. 5000/= na ujumbe uliosema “ I love you baby “.... Nilipofika
nyumbani nikawapigia rafiki zangu simu nikawaeleza, walishtuka sana, wengine
waliniambia namsingizia .
"Rafiki yangu Hawa akanishauri nibadilishe laini siku
hiyo hiyo na pale saluni nisikae. Nikanunua laini mpya , nikaenda kutafuta kazi
ya saluni Yombo pale kwangu nikaweka msichana.
"Nikamwambia mtu yoyote akiniuliza amwambie nimesafiri
na simu sina. Na kweli huyo mama alikuwa anakuja mara kwa mara saluni kwangu
kuniulizia , lakini hakupata mafanikio yoyote.
"Matokeo yake niliamua kuhama nikapangisha nyumba yangu
nikahamia Tandika nyumbani kwetu. Nilicho hofia ni kwamba kwa sababu nilishakula
pesa yake nyingi, angefikia kunitaka kimapenzi, matokeo yake ningemkatalia
angeweza kunifanyia chochote….
JE KITU GANI
KILITOKEA? ILIKUWAJE HADI ZUWENA
AKAAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI NA MWANAMKE HUYU MSAGAJI
?
NUNUA KITABU HIKI KUPITIA MTANDAONI KWA SHILINGI
ELFU TANO TU ( TSHS.5000/=) ZA KITANZANIA.
WASAMBAZAJI : MAMBO
COMMUNICATION
IDADI YA KURASA : KURASA THEMANINI ( 80
)
IDADI YA SURA (CHAPTERS ) : SURA
26.
BEI YA KITABU : SHILINGI ELFU TANO TU (
TSHS.5000/=)
UTARATIBU WA KUNUNUA KITABU
:
KITABU HIKI KINAUZWA KWA NJIA YA
MTANDAO.
NAMBA YA SIMU YA WAUZAJI WA KITABU HIKI
:
0766 101
669
0 comments: