SAKATA LA USAGAJI LAENDELEA KUWASUMBUA MASTAA WA BONGO..HIKI NDICHO KILICHOMKUTA DIDA WA TIMES FM ..SOMA HAPA KUJUA
Stori: Richard Bukos
DUNIA ina mambo! Prizenta wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’
amezua timbwili baada ya kung’ang’aniwa na mwanamke mwenzake aliyedaiwa
kutaka kumshawishi afanye naye mapenzi ya jinsi moja (usagaji).
Dida alikumbwa na ishu hiyo, Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya
Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, wakati Kundi la Mashauzi
Classic, lilikuwa likiangusha burudani.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina moja la Addy ambaye anadaiwa kukubuhu kwa tabia hiyo chafu ya usagaji. Ilisemekana kwamba mwanadada huyo alianza kumzengea Dida kwa kumsemesha huku akimuonesha pozi za kimahaba. Licha ya mtangazaji huyo kumpuuza, Addy alifika mbali na kuanza kumshtua kwa kutokea nyuma yake kwa kumtekenya huku akimkonyeza na kumshawishi waongee vizuri.
Kutokana na vitendo hivyo, Dida alipandwa na hasira na kuchukua chupa kutaka kumpasua ndipo Addy naye akawa anahangaika kujitetea na kusababisha vurugu katika eneo hilo, shukrani ziwaendee wasamaria wema waliwatuliza. Akizungumza na Risasi Jumamosi mara baada ya kutulizwa, Dida alisema:
“Huyu dada ni muda mrefu alikuwa akinisumbua hapa ukumbini, mwanzo nilikuwa sijajua anachotaka kumbe ni mshenzi kabisa, anataka kunifanya vitendo vya kisagaji, amenikera sana.” -GPL

0 comments: