NOMAAA.!! MSANII WA BONGOFLEVA AKUTWA AKIZINI NA MWANAFUNZI UFUKWENI..
Mara baada ya kunaswa, Bebuz alianzisha varangati kubwa lakini polisi jamii walimtuliza kwa virungu kisha kumfunga pingu na kumtaka atulize mzuka atoe ushirikiano vinginevyo angeumia.
Kijana huyo alitulia kwa muda lakini alipowaona OFM wakipiga picha, alilianzisha tena na kutaka kuvunja kamera huku akitamba kuwa alikuwa na uwezo huo.
Hata hivyo, OFM walikuwa makini kama kawaida yao.
Kikosi maalum cha kufichua maovu OFM (Opereshen Fichua Maovu) cha Global Publishers kilipiga kambi katika ufukwe huo kwa muda wa wiki moja na kushuhudia maovu yanavyofanyika.
Katika siku za hivi karibu, machangudoa wamekuwa wengi ufukweni hapo na baadhi yao ni vibaka ambao wamekuwa wakitoka nduki na nguo za wanaume huku wakisachi na kuchukua kila kitu.

0 comments: