MAPENZI YETU YALIANZIA BEACH, NA YAKAISHIA BEACH..! soma kwa makini kisa hiki cha kusisimua

Nilipoona vile nilienda nakumshika mmko huku akining'ang'ania kwa nguvu akiogopa kuzama, nilifanikiwa kumtoa nje. watu walipoanza kujaa aliamka nakujifanya kama hakuna lililotokea kwani hakutaka watu wengi kumjalia pale. Aliamka na kuoneka ahuko sawa tu. Alinishukuru sana na baadae akaniomba nijiunge nae siku ile. tulikaa eneo lile mpaka majira ya saa nne hivi usiku
Baadae tuliondoka pale akanipa lift na kunishusha kwangu kijitonyama, alipofika tu kwake alinipigia simu nakuendelea kunishukuru kwa yote. Basi mawasiliano yaliendelea hadi siku moja nakumbuka ilikuwa weekend alinipia simu nakuomba kuja kunisalimu, alipitia kwangu majira ya jioni hivi nikamkaribisha , alifungua mwenyewe fridge nakujimiminia mvinyo huku tukiendelea na story. Baada ya muda alianza kulewa na akaonekana ni mtu aliyechoka sana nilimkaribisha chumbani na kujitupa kitandani, na mimi nilijongea kumpa kampani. Nilianza uchokozi na mwishowe tukala tunda.
Baada ya tendo hilo, alipumzika kidogo nakuondoka, mapenzi yetu yaliendelea kwa muda wa miezi mitatu, Siku moja tulikubaliana twende beach kule kule tulipo onana nilichelewa kidogo kufika nikakuta yeye tayari yuko pale ananisubiri, alifurahi kuiona tukaka wote pale kwa muda sana.
Ilipofika jioni alipigiwa simu akawa ni kama mtu mwenye wasi wasi, huku akiongea na simu kwa woga kidogo, nakujielezea alipo huku akisema yuko sinza. Mmmh mi nikashtuka kidogo nakujiuliza kwa nini anadanganya na anaonekana mwenye wasiwasi. Mara tu akatokea jamaa mmoja mrefu aliyeonakana mweye hasira nakumuambia mpenzi wangu tuondoke, hukua akimuuliza kwa ukali kwanini unanidanganya, nakufanyia kila kitu na bado unanidanganya.
Niliogopa sana yule jamaa akanimbia "dogo ondoka kabla sijakumaliza" niliamka nakutoka nje nikachukua pikipiki na kurudi nyumbani. Kesho yake asubuhi yule msichana alinipigia simu akiniomba msamaha kwa yaliyotokea huku akidai yule ni mpenzi wake ila hampendi yuku tu nae kwasababu anamsaidia. Nikamuambia naomba usintafutie matatizo tuacha kabisa mawasiliano sitaki kabisa. Nikamkatia simu sasa ni mwezi wa nne toka tuachane ingiwa bado huwa ananikumbuka kwa simu na kuniomba nirudiane nae. Naombeni Ushauri wadau je nirudiane nae au nimpotezee

0 comments: