MAKUBWA HAYA..!! MSANII SNURA MUSHI AINGILIA KATI BEEF ZITO LA WEMA SEPETU NA KAJALA..
MSANII wa filamu na muziki, Snura
Mushi ameingilia kati ugomvi wa wasanii wenzake, Wema Sepetu na Kajala
Masanja na kuwaagiza wamalize tofauti zao.
Wasanii hao ambao wameingia kwenye bifu la kufa mtu kufikia hatua ya
kuanikana kwenye vyombo vya habari huku chanzo kikubwa kikitajwa ni
shilingi milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kajala kama faini ya kesi ya
kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa rehani kisheria iliyokuwa ikimkabili
mahakamani.
Nyumba hiyo iliwekwa rehani kutokana na mume wa Kajala, Faraja Agustino kushitakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu.
Snura amewataka Wema na Kajala kutoangalia nani ana makosa, wamalize tofauti zao.
“Nawashauri wenzangu wasigombane na kuwekeana vinyongo hiyo ni kama wanawapa watu faida,
nawaomba wamalize kwani haipendezi kabisa kwa jinsi walivyokuwa
wameshibana. Kama mmoja anaona amemkosea mwenzake ajishushe na kuomba
msamaha,” alisema Snura.
By Na Chande Abdallah na Mayasa Mariwata GPL
0 comments: