HII NI AIBU YA MWAKA..!! MKE AISHI NA WANAUME WAWILI CHUMBA KIMOJA..SOMA STORI NZIMA HAPA
DUNIA
ina kila kituko, kama hujawahi kukisikia omba Mungu akupe uzima! Mama
mmoja, aitwae Elizabeth Selestine, mkazi wa Kigogo-Mburahati, Dar
hivi karibuni alizua timbwili nyumbani kwake baada ya majirani, wajumbe
na ndugu zake kumjia juu kwa kitendo chake cha kuishi na wanaume
wawili kwenye chumba kimoja, Ijumaa lina mkasa kamili.
Elizabeth Selestine anayeishi na wanaume wawili.
Ndani
ya timbwili hilo, watu kibao walikuwepo, lakini muhimu sana ni mdogo
wa mwanamke huyo, Oscar Selestine (17) ambaye alianika kila kitu.
Mume wa ndoa.
“Baada
ya kuanzisha uhusiano na Juma, mwenye nyumba (baba wa Juma)
aliwafukuza akiogopa kuwa kwa tabia ya dada lisije likatokea balaa
kubwa. Hata mimi na mdogo wangu tuliishi kwa dada na shemeji.
“Dada
na shemeji wakahamia kwenye chumba kimoja nyumba ya jirani, dada
akaniambia mimi na mdogo wangu mwingine tuishi nao huku tukitafuta pa
kulala kwa sababu wao walipata chumba kimoja ambacho tulikuwa tunalala
wote, mimi, mdogo wangu, dada, shemeji na watoto wao wawili.
“Lakini
siku moja nilishangaa kumwona Juma akija na godoro hapo hapo kwenye
chumba kimoja huku shemeji akiwemo,” alisema Oscar na kuwashangaza hata
mapaparazi. Dunia ina mambo mengi.
Mama mwenye nyumba.
“Nilishtuka
sana! Kulala kwenyewe, shemeji na dada kitandani, Juma akawa analala
chini wakati na yeye ni mtu mzima tena ana watoto,” alisema Oscar.
Oscar
aliendelea kusema kuwa, siku moja alishangaa kumwona Juma akimpiga
dada yake, alipojaribu kuuliza dada huyo akamjibu: “We mtoto,
hayakuhusu.” Mwisho yeye na mdogo wake wakafukuzwa na kuambiwa
wasifike nyumbani hapo.
Oscar
hakuona sababu ya kufunga kinywa bila kumalizia kusema yote, akaanika
kwamba ilifika mahali Juma alianza kumpiga shemeji yao kisa eti amekuwa
na wivu kwa mke wake. Makubwa hayo!
“Kumbe
mtoto mmoja wa dada alikuwa akiona kila kitu, siku moja akaanika siri
kwamba, Juma huwa anampiga shemeji usiku na ili amuache dada alale naye
chini,” alisema Oscar.
Ndugu wa mke.
Oscar
akasema hakuna siri ya watu wawili, baadaye habari zilizagaa kwa ndugu
wote kuwa dada yao anaishi na wanaume wawili, ndipo mama mwenye nyumba
alimuita na kumkanya lakini hakusikia.
Mwenye
nyumba alipoona jeuri hiyo alimuita tena na kumpa siku saba aondoke
ndani ya nyumba yake lakini bado Elizabeth hakufanya hivyo.
Oscar
tena: “Huwezi amini ilifika wakati shemeji akileta chakula kinapikwa
halafu yeye hatengewi, anatengewa Juma, shemeji akiuliza anaambiwa akale
na watoto. Sisi hatumuelewi shemeji, kama ni madawa basi yamemkolea
sana.”
Ikadokezwa
kwamba tukio hilo lilifika mbali, hadi kwa wazazi wa mwanaume,
Kilosa, Morogoro ambao walifunga safari mpaka Dar lengo lilikuwa
kuwachukua wajukuu na mtoto wao Benedicto, lakini ilishindikana kwani
waliambulia kutukanwa na mwanamke huyo, wakaondoka wakiacha laana
nyuma.
Vituko viliendelea siku hadi siku, siku moja
Benedicto au maarufu kwa jina la ‘baba Gire’ alikwenda kwa mjumbe wa
eneo hilo, Maua Thabiti huku akilia na kuapa ipo siku atafanya kitu
kibaya ambacho mkewe na Juma hawatakaa wakisahau.
Mjumbe
huyo ambaye ni wa shina namba 48, mtaa wa National Housing Mburahati,
Dar alikiri kupokea malalamiko hayo lakini akasema mwanaume huyo
anaogopa kuweka wazi kwa sababu atapigwa, hivyo anamuachia Mungu.
Mwenye nyumba wanayoishi watu hao, Flora Mtumbati alipoulizwa naye alikiri kuwa, Eliza anaishi na wanaume wawili.
“Baada
ya kubaini hilo, Eliza aliitwa na Jumuiya ya Katoliki anakosali na
kuonywa. Mimi nilimpa siku saba za kumtoa Juma na kubaki na mumewe,
aliniahidi lakini hakufanya hivyo, bora watu wa magazeti mmekuja mnaweza
kunisaidia,” alisema Flora.
Baada ya kuongea na vyanzo vyote, gazeti lilimtafuta Elizabeth:
“Huyu
bwana (Juma) alikuja kwangu kwa matatizo, alikaribishwa na mume wangu,
nilimkaribisha chumbani kwangu kwa sababu ndiyo chumba hichohicho.
Hata hivyo, leo (Ijumaa iliyopita) anahama.”
Baada
ya waandishi kuondoka, mwanamke huyo alitishia kujiua. Siku ya pili,
waandishi waliambiwa kuwa mwanamke huyo alikimbilia Kimara kwa wifi
yake ambaye ni ndugu wa Juma.
Benedicto alipopatikana alisema: “Sikuamini kama mke wangu anatembea na Juma ingawa niliwahi kusikia.
Kuhusu kupigwa ni kweli hasa akilewa pombe. Baada ya sakata hili mke
wangu amesema kwa watu kuwa hata mtoto wa mwisho si wangu, ni wa Juma.
Inauma sana.”
Baada
ya waandishi kuibua ishu na watu kujaa, inadaiwa Juma alitafuta
vijana na kumpa kichapo cha nguvu baba Gire ambapo ameshonwa nyuzi kumi
na mbili mdomoni na jichoni.
Kesi hii ilifikishwa Kituo cha Polisi Mburahati na kufunguliwa jalada namba MBR/RB/1204/13 KUJERUHI.
0 comments: